Baada ya benki kubwa kadha wa kadha za kimataifa kusitisha shughuli zao Côte d'Ivoire, Benki ya Afrika na Benki ya Kimataifa ya Afrika Magharibi tarehe 18 pia zimesimamisha shughuli zao nchini humo, ambapo hali ya watu wengi kuchukua akiba zao haraka imetokea katika benki nyingine za Cote dIvoire ambazo bado hazijafungwa.
Hivi sasa, Misururu mirefu ya watu wanaotaka kuchukua pesa zao imeonekana kwenye benki kadhaa huko Abidjan. Kutokana na sababu ya usalama, matawi ya benki za Ufaransa, Uingereza na Marekani nchini humo wiki hii yatasimamisha shughuli zao kwa nyakati tofauti.
0 comments:
Post a Comment