Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD linasema kuwa uwekezaji wa kigeni ulipungua mwaka uliopita wa 2010.
Hata hivyo nchi zinazoendelea zilishuhudiwa kuongezeka kwa uwekezaji wa kigeni. Mataifa ya Asia na Amerika kusini yalishuhudia uwekezaji mkubwa huku nchi za bara ulaya zikishudiwa kiwango kidogo cha uwekezaji wa kigeni. UNCTAD inasema kuwa kumeshuhudiwa mabadiliko katika kujiunga na uwekezaji wa kigeni tangu kuanza kushuhudiwa kwa hali mbaya ya uchumi duniani . Hata hivyo linasema kuwa uwekezaji huo unatarajiwa kuongezeka mwaka huu wa 2011.
0 comments:
Post a Comment