Searching...
Monday, January 10, 2011

Upigaji kura za maoni kusini mwa Sudan waanza

Upigaji kura za maoni kusini mwa Sudan umeanza saa mbili asubuhi ya leo tarehe 9. Upigaji kura huo utakaodumu kwa wiki moja, utaamua kama sehemu ya Kusini itajitenga na Sudan au la.
Watu karibu milioni 4 wa sehemu ya kusini mwa Sudan wanapiga kura katika sehemu mbalimbali nchini humo na katika nchi nane za nje.
Askari wapatao elfu 60 wanashughulikia ulinzi wa usalama, na waangalizi zaidi ya elfu 10 wa nchi hiyo na wengine zaidi ya 1,500 wa kimataifa wanaangalia upigaji kura huo, ili kuhakikisha upigaji kura huo unafanyika kwa uwazi na haki.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!