Searching...
Monday, January 10, 2011

Safari ya Hillary Clinton katika nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi

 Hillary Clinton Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani amewasili katika eneo la Mashariki ya Kati kwa shabaha ya kufuatilia siasa za uingiliaji kati za Washington katika eneo. Taarifa zinasema kuwa, Clinton atazitembelea nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman na Qatar katika ziara yake ya siku tano katika eneo. Hii inahesabiwa kuwa safari yake ya pili katika eneo, katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Taarifa zinasema kuwa, lengo la safari ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani katika eneo ni kuwashawishi viongozi wa nchi za Kiarabu kutumbukia kwenye ushawishi wa Washington wa kuiwekea vikwazo zaidi Iran. Weledi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa, zikiwa zimesalia siku kumi tu kabla ya kufanyika duru ya pili ya mazungumzo kati ya Iran na nchi wanachama wa kundi la 5+1 huko Uturuki, haitarajiwi kwamba Washington itaingia kwenye mazungumzo hayo ikiwa na nia njema na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!