Searching...
Tuesday, January 11, 2011

Odinga: Mapinduzi ya kijeshi yatarejea Afrika

 Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kuwa mgogoro wa kisiasa ambao umeshindwa kutatuliwa na Ivory Coast yumkini ukadumaza na kurejesha nyuma demokrasia barani Afrika.
Odinga ameashiria chaguzi zinazotarajiwa kufanyika katika nchi kama Nigeria na Uganda na kutahadharisha kwamba huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo kiongozi anayeng'ang'ania madaraka wa Ivory Coast hatalazimishwa kuondoka madarakani. Amesema kuna uwezekano hali ya vurugu na ukosefu wa imani kuhusu uwezekano wa kuhamishwa madaraka kupitia masunduku ya kupigia kura ikapelekea kurejea mapinduzi ya kijeshi barani Afrika. Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye ni mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika katika mgogoro wa Ivory Coast amesema majeshi sasa yatakuwa yakitwaa madaraka kwa kisingizio cha kurejesha amani na nidhamu.
Zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha katika ghasia za baada ya uchaguzi wa rais nchini Ivory Coast na juhudi zinaofanywa kutatua mgogoro wa nchi hiyo zimeshindwa hadi sasa. Jamii ya kimataifa inamtaka Laurent Gbagbo akabidhi madaraka ya nchi kwa hasimu wake wa kisiasa Alassane Ouattara ambaye alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais nchini Ivory Coast

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!