Viongozi wa makabila ya kaskazini ya Misseriya na wale wa kusini Ngok Dinka waliendelea kutupiana shutuma jumatatu juu ya kuendelea kwa ghasia katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei ambalo linapiganiwa kati ya mpaka wa kaskazini na kusini.
Msemaji wa umoja wa mataifa Martin Nesirky amesema askari walinda amani wa umoja wa mataifa wameongeza doria katika eneo la Abyei. Amesema umoja wa mataifa umeguswa sana na ghasia na wapo katika hatua ya kuthibitisha idadi ya majeruhi.
0 comments:
Post a Comment