Searching...
Sunday, January 9, 2011

Johannesburg-Afrika Kusini yaunda kikundi maalumu ili kushughulikia wahamiaji wa Zimbabwe

Idara kuu inayoshughulikia mambo ya wahamiaji ya wizara ya mambo ya ndani ya Afrika Kusini tarehe 7 ilitoa taarifa, ikisema imeanzisha kikundi maalumu, ili kushughulikia maombi ya visa ya wazimbabwe nchini Afrika Kusini.
Inakadiriwa kuwa hivi sasa idadi ya wazimbabwe wanaoishi nchini Afrika Kusini ni karibu milioni tatu, na kati yao watu wengi hawana visa halali. Serikali ya Afrika Kusini inawataka watu hao wapate visa kabla ya tarehe 31, Desemba mwaka 2010, na hadi mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, wizara ya mambo ya ndani ya Afrika Kusini ilikuwa imepata maombi zaidi ya milioni 1.5 ya visa kutoka wazimbabwe.
Taarifa hiyo inasema kazi ya kupitisha mambo hayo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu, na kabla ya hapo, Afrika Kusini haitawafukza wazimbabwe nchini humo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!