Searching...
Sunday, January 9, 2011

China yapenda kushirikiana na Umoja wa Ulaya kukabiliana na msukosuko wa uchumi

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na msukosuko wa uchumi unaoukabili umoja huo kwa muda, ili kupata maendeleo ya pamoja.
Bw. Li Keqiang aliyasema alipokuwa na mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Amesema hali halisi inaonesha kuwa China na Ujerumani zinaweza kuwa wenzi wanaotegemeana, na bado kuna nguvu kubwa ambayo haijatumika ipasavyo katika kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Bibi Angela Merkel amesema Ujerumani inapenda kufanya mazungumzo na China katika mambo ya siasa, uchumi, diplomasia, sayansi, uhifadhi wa mazingira na jamii, na itafanya kazi kubwa katika kuuhimiza Umoja wa Ulaya uitambue hadhi ya uchumi wa soko huria ya China.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!