Searching...
Thursday, January 6, 2011

China yashindwa kupiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya nyumba


China ikiwa nchi iliyosaini Mkataba wa Shirika la Afya Duniani WHO unaohusu Udhibiti wa Matumizi ya Tumbaku, imeshindwa kuzuia uvutaji wa sigara kwenye maeneo yote ya umma yaliyo ndani ya nyumba, yakiwemo ofisi na vyombo vya usafari wa umma, kama inavyotakiwa kwa mujibu wa mkataba huo.
Mkurugenzi wa ofisi ya taifa ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku Bibi Yang Gonghuan amesema, China inatakiwa kufikia matakwa hayo kabla ya tarehe 9 Januari mwaka huu, miaka mitano baada ya kuanza kufanya kazi kwa mkataba huo. Bibi Yang amesema kuwa, hivi sasa China bado haijatoa sheria ya taifa ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya umma na ofisi, na kwamba sera za hivi sasa bado hazitekelezwi vizuri. Pamoja na maelekezo yenye makosa kutoka kwenye makampuni ya tumbaku, kazi ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku inafanyika kwa taabu sana.
China ni nchi inayozalisha na kutumia tumbaku kwa wingi, pia ni nchi inayoathiriwa vibaya zaidi na matumizi ya tumbaku. Inakadiriwa kuwa nchini China kuna wavutaji wa sigara wapatao milioni 350, na wengine wapatao milioni 540 wanaathiriwa moja kwa moja na uvutaji wa sigara, na kila mwaka zaidi ya watu milioni moja wanakufa kutokana na maradhi yanayohusiana na uvutaji wa sigara.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!