Searching...
Friday, January 21, 2011

China yasamehe asilimia 50 ya madeni ya ujenzi wa reli ya TAZARA

Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan akiiwakilisha serikali ya China amesaini makubaliano na wajumbe wa serikali za Zambia na Tanzania kuhusu kusamehe asilimia 50 ya madeni ya ujenzi wa reli ya TAZARA tarehe 19 usiku huko Lusaka.
Bw. Zhong Shan amesema serikali ya China imeamua kusamehe baadhi ya madeni ya ujenzi wa reli hiyo kutokana na urafiki wa jadi kati ya China na nchi za Afrika, na watu wa China wanapenda kufanya kadiri wawezavyo kuwaunga mkono watu wa Afrika katika maendeleo ya uchumi na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.
Waziri wa fedha na mpango wa Zambia Bw. Situmbeko Musokotwane aliishukuru serikali ya China akisema, serikali ya Zambia itashirikiana na serikali za China na Tanzania kuhakikisha uendeshaji wenye ufanisi zaidi wa reli hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!