Searching...
Saturday, January 1, 2011

Mwaka mpya 2011 wakaribishwa kwa mlipuko nchini Nigeria

Watu wasiopungua 30 wameuawa na kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye kambi moja ya jeshi katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Polisi imesema kwamba mlipuko huo umetokea katika kambi ya jeshi ya Sani Abacha wakati watu walipokuwa wamekusanyika kusherehekea kuingia mwaka mpya usiku wa kuamkia leo. Mlipuko mwingine ulitokea katika soko la Mamy wakati watu walipokuwa wakila na kunywa.
Bado sababu za milipo hiyo hazijajulikana. Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametoa amri kwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuwasaka na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa milipuko hiyo. Wiki iliyopita pia kulitokea milipuko kadhaa katika mji wa katikati mwa Nigeria Jos na ule wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wa Maiduguru.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!