Ndege ya mwisho iliyobeba waislamu wa China waliokwenda kuhiji iliondoka Jeddah, Saudi Arabia na kurudi Beijing tarehe 14 usiku. Waislamu hao 330 walitoka mikoa ya Yunnan, Shandong na Hainan. Mpaka sasa waislamu elfu 13 wa China wamekamilisha hija kwa mwaka huu.
Maofisa husika wa idara ya mambo ya dini ya China na shirika la dini ya Kiislamu la China waliwalaki watu hao kwenye uwanja wa ndege na kuwapongeza kwa kukamilisha hija.
0 comments:
Post a Comment