Searching...
Friday, December 10, 2010

Ufisadi watishia maendeleo, utulivu na demokrasia :Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ufisadi ni kitishio kikubwa kwa maendeleo na demokrasia. Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya kupambana na ufisadi Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kila uwezalo kuhakikisha kuwa ufisadi umeangamizwa kote duniani.
Ban pia amesema kuwa ufisadi ni chamgamoto kwa ukuaji wa uchumi na pia unazuia uwekezaji wa kigeni. Ameongeza kuwa ufisadi unachangia kuharibika kwa mazingira na kuzorota kwa afya kupitia kuruhusu kutupwa ovyo kwa taka na kuundwa kwa madawa bandia. Ban amewataka viongozi wa kibiashara wanaopinga ufisadi pia kuambatanisha matamshi yao na vitendo kwa kuzingatia sera zinazopinga ufisadi kulingana na makubalino ya Umoja wa Mataifa kuhusu ufisadi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!