Searching...
Tuesday, December 7, 2010

Nchi za Kiarabu zataka suala la nyuklia la Iran litatuliwe kwa amani

Katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa itaendelea kufanya mazungumzo na kundi la 5+1 chini ya msingi wa mkataba wa NPT, Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Ujemi limetaka suala la nyuklia la Iran litatuliwe kwa njia za amani.
Kikao cha Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kilifunguliwa jana mjini Abu Dhabi Imarati kwa mwito wa kutatuliwa kwa njia za amani suala la nyuklia la Iran na kutoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel usimamishe ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na uruhusu kuundwa nchi huru ya Palestina.
Kikao cha siku mbili cha mjini Abudhabi kimefunguliwa na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zaid Aal Nahyan.
Wakati huo huo Said Jalili Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza tena kwamba haki za Iran katika suala la nyuklia kamwe haziwezi kuwa ajenda ya mazungumzo hayo ya Tehran na kundi la 5+1 linaloundwa na Uingereza, China, Ufaransa, Russia, Marekani pamoja na Ujerumani. Mazungumzo hayo yaliyoanza jana Jumatatu yanaendelea leo huko Geneva Uswisi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!