Searching...
Wednesday, December 22, 2010

Mlipuko wa mabomu ya mkononi watokea Nairobi

Ofisa mhusika wa kampuni ya mabasi ya abiria tarehe 20 alithibitisha kuwa, mlipuko wa mabomu ya mkononi umetokea katika basi lililokuwa likielekea Kampala Uganda kutoka Nairobi siku hiyo usiku na kusababisha kifo cha abiria mmoja na wengine 26 kujeruhiwa.
Akithibitisha tukio hilo, ofisa huyo alisema, ndani ya basi hilo kulikuwa na abiria 30 hivi. Wakati abiria wengine wakiendelea kupanda, ghafla watu wanne walitaka kuingia kwenye basi hilo bila kufuata taratibu, na wakaguzi wa usalama walipowazuia kuingia, watu hao walitupa begi lililokuwa na mabomu ya mkononi ndani ya basi hilo, ambayo yalilipuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wengi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!