Maharamia wa Somalia wameiteka nyara meli iliyokuwa na bendera ya Panama ya Mv Renuar baada ya kuishambulia kwa silaha ndogo ndogo na maroketi. Kikosi cha majini cha Umoja wa Ulaya kimeripoti kuwa Mv Renuar ni meli ya kubeba mizigo inayomilikiwa na Liberia iliyokuwa na shehena yenye uzito wa tani 70,156. Meli hiyo ilitekwa nyara na maharamia jana wakati ikielekea Fujairah katika Umoja wa Falme za Kiarabu ikitokea katika bandari ya Louis huko Mauritius. Maharamia hao wamethibitisha kuchukua udhibiti wa meli hiyo ambayo sasa inaelekea katika pwani ya Somali.
Maharamia wa Somalia waiteka nyara meli ya Panama

0 comments:
Post a Comment