Searching...
Thursday, November 4, 2010

UM na washirika wake watoa ombi la dola milioni 47 kuwasaidia walokumbwa na mafuriko Benin

Mashirika ya miasaada yanayosaidia nchini Benini kukabiliana na athari za mafuriko yamezindua ombio la msaada wa dola milioni 47 ili kuwanusuru maelfu ya watu waliosambaratishwa na mafuriko hayo.
Mafuriko Benin
Mafuriko Benin
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa masuala ya kibinadamu OCHA imesema mvua kubwa zilizonyesha katikati ya mwezi septemba zimesababisha mafuriko na maafa makubwa katika nchi nzima ya Benin. Zaidi ya watu 680,000 katika majimbo 55 kati ya majimbo 77 ya nchi hiyo wameathirika.
Elizabeth Byrs msemaji wa OCHA anasema msaada wa fedha unahitajika haraka, kwa ajili ya kupata chakula, madawa na kufanyia ukarabati shule zilizoharibiwa, hospitali na barabara.

Nchi nyingi za Afrika ya Magharibi na Afrika ya kati zinakabiliwa na mafuriko mabaya kabisa kuwahi kutokea kwa miaka mingi. Zaidi ya watu milioni 1.8 wameathirika.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!