"Tumehesabu matokeo ya kila kituo na kulinganisha na matokeo yanayotolewa vituo vya kata, wilaya na ya kitaifa na kuna kasoro chungu nzima, "amesema Dk Wilbrod Slaa.
Hadi Jumatano jioni tume ya uchaguzi imekua ikitoa matokeo ya sehemu kadhaa ya uchaguzi na haikutoa matamshi yeyote kutokana na madai ya upinzani. Kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo yamesababisha kuzuka kwa hali ya wasi wasi katika kila pembe ya nchi na watu kuanza kuuliza kwanini inachukua muda huu wote kutangaza matokeo hayo.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kuwepo na mvutano mkubwa katika kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais huko Tanzania tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1995.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Dk Slaa anasema, "nimesoma ripoti ya awali ya wafuatiliaji wa kimataifa na wamesema taratibu nyingi zimekiukwa, lakini sijui ni taratibu gani kwa sababu taarifa yao kina haijatoka, nimesoma tu kwenye magazeti".
Lakini anasema jambo muhimu la kufahamu ni kwamba wafuatiliaji wa kimataifa hawafanyi kazi ya kina kama wanavyofanya wao.Kwani anasema wanachukua matokeo ya kila kituo na kuhesabu upya na kulinganisha na matokeo ya tume ya taifa na wameshuhudia kasoro nyingi.
0 comments:
Post a Comment