Searching...
Wednesday, November 24, 2010

Nairobi-Idadi ya watu kwenye miji barani Afrika yakadiriwa kuongezeka kwa mara mbili

Ripoti mpya kutoka Shirika la makazi la Umoja wa Matifa (UN-HABITAT) imesema, katika miaka 40 ijayo idadi ya watu kwenye miji barani Afrika itaongezeka na kufikia mara tatu kuliko ya hivi sasa, na miji ya nchi za Afrika pia itakabiliwa na athari mbalimbali kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya watu kwenye miji barani Afrika inaongezeka kwa zaidi ya asilimia 4 kwa mwaka, na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030, idadi ya watu kwenye miji itachukua zaidi ya asilimia 53 ya idadi ya juma ya watu wa Afrika. Na kasi kubwa ya kupanuka kwa miji imekuwa changamoto kubwa ya usimamizi kwa serikali katika nchi za Afrika.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!