Searching...
Monday, November 8, 2010

Maandalizi ya michezo ya Asia yakamilika


Zikiwa zimebaki siku tano kabla ya kufunguliwa kwa michezo ya 16 ya Asia itakayofanyika huko Guangzhou, kusini mwa China, kamati ya maandalizi ya michezo hiyo imesema, maandalizi ya michezo hiyo yamekamilika. Imefahamika kuwa michezo hiyo ya Asia itashirikisha wanamichezo 10,156 kutoka nchi na sehemu 45, na ratiba ya michuano yote 630 imepangwa na kutangazwa hadharani.
Katika upande wa uwanja wa michezo, viwanja 53 vya michezo na vingine 17 vya mazoezi viko tayari na vimefunguliwa kwa wachezaji kuanzia tarehe 5 Novemba, na vifaa vyote vya michezo tayari vimefungwa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!