Searching...
Monday, October 25, 2010

Shemeji yake Blair asilimu baada ya kuzuru Haram ya Bibi Maasumah Qum

 Lauren Booth dada wa Cherie Blair mke wa Tony Blair Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza amesilimu mara baada ya kuzuru Haram ya Bibi Fatimat Maasumah Alayha Salaam katika mji wa Qum. Taarifa zinasema kuwa, Lauren Booth mwenye umri wa miaka 43 hivi sasa anavaa vazi la stara la mwanamke wa Kiislamu Hijab na kushiriki kwenye sala za jamaa Msikitini. Lauren Booth ameongeza kuwa, hivi sasa amefungamana na sheria za Kiislamu kwa kuacha kula nyama ya nguruwe na kunywa pombe. Ameongeza kuwa, alichukua uamuzi wa kusilimu yapata miezi sita iliyopita, baada ya kufanya utafiti juu ya itikadi ya dini ya Kiislamu. Hata hivyo Booth alimuandikia Blair barua kali na kumueleza kuwa, mtazamo wenu Wamagharibi kuhusiana na ulimwengu ni huu kwamba; Waislamu ni wendawazimu, wabaya na hatari. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Booth akiwa pamoja na wanaharakati wengine 46 wa kutetea haki za binadamu walielekea Ukanda wa Gaza, kwa shabaha ya kuvunja mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel mnamo mwaka 2008.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!