Searching...
Monday, October 25, 2010

China yafurahia ushirikiano wa kimkakati kati ya UN na AU

China imeeleza kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuanzisha na kuendeleza ushirikiano wa kimkakati. Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Li Baodong amesisitiza msimamo huo wa China kwenye mjadala ulioitishwa tarehe 22 na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuchangia shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Afrika.
Balozi Li alisema katika miaka ya hivi karibuni Umoja wa Afrika umekuwa unafanya kazi muhimu katika kulinda amani na utulivu wa Afrika na kutatua migogoro barani humo, lakini pia unakabiliwa na matatizo ya fedha katika kutekeleza majukumu hayo, ndiyo maana unahitaji msaada wa haraka kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa. Balozi huyo aliongeza kuwa, China inaona Umoja wa Mataifa unatakiwa kuusaidia Umoja wa Afrika katika kupata fedha za uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya kulinda amani.
Kwenye mjadala huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon alisema, katika kutekeleza jukumu la kulinda amani linalokubaliwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika unastahili kupata uungaji mkono unaolingana na majukumu mengine ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, zikiwemo pensheni kwa walinzi amani. Bw. Ban Ki-Moon aliongeza kuwa, pamoja na kuusaidia Umoja wa Afrika katika kuimarisha uwezo wake wa kutekeleza jukumu la kulinda amani, cha muhimu ni kuhakikisha unapata vitu vinavyohitajika katika kukamilisha jukumu hilo. Pia alitoa pongezi kwa Umoja wa Afrika na mashirika ya kikanda ya Afrika kutokana na kufanya jitihada kubwa katika kuzuia, kuisuluhisha na kuiondoa migogoro. Bw. Ban Ki-Moon alisema kuimarisha mfumo wa amani na usalama barani Afrika kunafanya kazi muhimu sana katika kutatua na kuzuia migogoro kwa ufanisi na kwa upeo wa mbali.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!