Searching...
Monday, October 11, 2010

Mke wa mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani awekwa kizuizini.

 
Mke wa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2010, Liu Xiaobo, bibi Liu Xia.

Mke wa mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel Liu Xiaobo, bibi liu Xia amezuiliwa nyumbani kwake mjini Beijing.


Msemaji wa Shirika la haki za binadamu la Marekani lenye makaazi yake nchini China, amesema Bibi Liu Xia amewekwa katika kizuizi cha nyumbani.
Alikuwa amekwenda kumtembelea mume wake gerezani ili kumpa habari za ushindi wa tuzo ya amani na kwamba aliporudi nyumbani kwake mjini Beijing alizuiwa asitoke.
Liu Xiaobo. Liu Xiaobo alishinda tuzo ya amani ya Nobel siku ya Ijumaa kutokana na miongo miwili ya harakati zake zisizotumia nguvu ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa nchini China.
 

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!