Searching...
Thursday, September 23, 2010

Wakenya wataka mashitaka ya ICC

Mwanajeshi akimkwida mtu wakati wa ghasia
Madai yanayotokana na ghasia za uchaguzi 2008 hayajafanyiwa kesi.
Matokeo ya utafiti mpya yanaonyesha kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Kenya wanataka Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuwafanyia kesi watuhumiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Kulingana na matokeo yaliyotolewa Jumanne, asilimia 54 ya Wakenya wanapendelea ICC iendeshe kesi hizo badala ya mahakama za ndani ya Kenya.
Miongoni mwa wale wanaopinga uingiliaji wa ICC nusu wanasema wanataka watuhumiwa wafanyiwe kesi na mahakama za ndani ya nchi, na nusu wanasema ni bora wasamehewe.
Jumapili, Waziri wa Sheria wa Kenya, Mutula Kilonzo, alizusha mzozo alipopendekeza kuwa Kenya inaweza kuendesha kesi dhidi ya watuhumiwa hao kwa kupitia taasisi zilizoundwa na katiba mpya ya Kenya.
Matamshi ya Kilonzo yalipingwa vikali na makundi ya haki za binadamu na hata maafisa wengine wa serikali.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!