Searching...
Wednesday, September 29, 2010

Serikali ya Kenya yawaomba wabunge kuunga mkono miswada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Sample ImageSerikali ya Kenya imewaomba wabunge wa nchi hiyo kuunga mkono miswada inayolenga kuimarisha nafasi ya nchi hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakizungumza muda mfupi kabla ya kuanza rasmi vikao vya bunge baada ya likizo ya mwezi mmoja, Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Waziri anayehusika na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Hellen Sambili wamesema kuwa serikali inatayarisha miswada 28 inayolenga kuimarisha uhusiano wa Nairobi na Jumuiya hiyo na hivyo kuwataka wabunge kuunga mkono na kuipitisha miswada hiyo.
Profesa Hellen Sambili amesema kuwa kuanza protokali ya soko la pamoja la EAC mwezi Julai mwaka huu ni nafasi nzuri ya Kenya kuimarisha satua yake ya kibiashara katika eneo hilo lakini akatahadharisha kuwa endapo miswada hiyo haitapitishwa basi azma hiyo itakuwa vugumu kutekelezeka.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!