Searching...
Wednesday, September 29, 2010

Kenya yaweka mkakati wa kuwatambua wafadhili wa kundi la Al-Shabab

 Sample ImageBenki Kuu ya Kenya CBK imeziamuru benki zote nchini humo kufuatilia kwa karibu shughuli za kibiashara za baadhi ya wafanyabiashara wenye asili ya Kisomali ambao wanashukiwa kuwa wanalifadhili kundi la wanamgambo wa Al-shabab la nchini Somalia. CBK imesambaza majina ya wafanyabiashara hao ambayo pia yamo kwenye orodha ya watu wanaoshukiwa na Umoja wa Mataifa kufadhili kundi hilo. Benki za Kenya zimetakiwa kuwa macho na kuchunguza orodha hiyo ya UN kila mara na kufuatilia kwa karibu biashara zinazozidi dola 10,000. majina yaliyoko kwenye orodha ya UN pia yanamjumuisha kiongozi wa kundi moja la waasi nchini Somalia Sheikh Hassan Dahir Aweys. Wanamgambo wa Al-Shabab wanapigana kufa kupona ili kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia inayoongozwa na Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!