Searching...
Monday, September 20, 2010

Nairobi-China na Kenya zaanza ukaguzi wa mabaki ya kale chini ya bahari

Idara ya ukaguzi wa mabaki ya kale ya sehemu za pwani ya Jumba la makumbusho ya Kenya tarehe 19 ilitangaza kuwa, ushirikiano kati ya China na Kenya katika ukaguzi wa mabaki ya kale chini ya bahari utaanza tarehe 27 Novemba mwaka huu kisiwani Lamu mashariki mwa Kenya. Mradi wake ni kuibua meli zilizozama katika bahari iliyoko karibu na kisiwa cha Lamu wakati baharia Zheng He aliposafiri Afrika Mashariki.
Msaidizi Mkurugenzi wa idara hiyo Bw. Atame Hussein siku hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, wataalamu watatu wa China na wawili wa Kenya watashiriki pamoja kwenye ukaguzi wa mabaki ya kale chini ya bahari utakaofanyika mwezi Novemba.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!