Searching...
Wednesday, September 22, 2010

Marekani yahimiza Sudan kutekeleza mkataba wa amani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton akutana na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, mwenyekiti wa Jopo la AU juu ya Sudan na mwakilishi maalum wa UM kwa ajili ya Sudan Haile Menkerios.
Marekani imeisihi Sudan kutekeleza majukumu yake kwa mujib wa mkataba wa amani na kuitisha kura ya maoni.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani,  P. J.  Crowley, aliwaambia waandishi wa habari pembeni ya mikutano ya mwaka kwenye Umoja Mataifa waziri wa mambo ya nje, Hillary Clinton alikutana mapema Jumatatu na makamu rais wa Sudan, Ali Osman Taha.
Bwana Crowley amesema waziri Clinton amethibitisha nia ya dhati ya Marekani katika utekelezaji kamili wa mkataba huo na kurejea kwamba kuna haja ya kuona hatua zinachukuliwa ili kuhakikisha   kuwa  kura ya maoni inaitishwa kwa wakati   muafaka kwa ajili ya  wote  Sudan kusini na na Abyei ili kuunga mkono mkataba huo wa amani.
Mkataba wa amani wa mwaka 2005 ulimaliza vita virefu vya Sudan vilivyodumu kwa  miongo miwili  kati ya kaskazini na kusini.
Msemaji Crowley amesema makamu rais Taha alirejea  nia ya dhati ya Khartoum  kwa mkataba huo, na kukiri kuwa kuna mengi yanahitaji kufanywa kabla ya upigaji kura wa January.
Wanadiplomasia wa magharibi kwenye Umoja Mataifa katika wiki za karibuni walielezea wasi wasi kwamba matayarisho kwa kura hiyo yamekwama. Wana wasi wasi kwamba kuakhirisha upigaji kura, ama kunaweza kuonekana kuwa  pengine matokeo yasingekuwa ya  uhakika  na hii  huenda ikairejesha nchi katika ghasia.
Msemaji wa Marekani amesema Washington itampeleka Princeton Lyman, mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani katika eneo hilo wiki ijayo, wakati uwakilishi wa Marekani umeongezeka huko na kuzidisha kazi zake na pande husika. Crowley amesisitiza umuhimu wa Sudan kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wa amani na kusema kutakuwa na madhara kama hilo halitafanyika.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!