Searching...
Tuesday, August 17, 2010

Umoja wa Mataifa watahadharisha kuwa ‘wimbi la pili la vifo’ linaloijongelea Pakistan

Tuesday, 17 August 2010 Sample ImageUmoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa Pakistan inajongelewa na kile ulichokiita ‘wimbi la pili la vifo' huku mashirika ya misaada yakifanya bidii za kukusanya fedha kuwasaidia watu milioni 20 walioathiriwa na janga kubwa zaidi la kimaumbile kuwahi kuikumba nchi hiyo. Wakati Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutolewa msaada wa dola milioni 460, mashirika ya misaada yamesema kumekuwepo na hali ya kusuasua katika kuitikia wito huo, huku manusura wa mafuriko nchini Pakistan wakiishutumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia. Maurizio Giuliano, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinaadamu (OCHA) amesema ana hofu ya Pakistan kukumbwa na wimbi la pili la vifo endapo haitopatikana misaada zaidi ya fedha kutoka kwa wafadhili na kuongeza kuwa watu wapatao milioni sita wakiwemo watoto milioni 3.5 wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na magonjwa yanayosababishwa na utumiaji wa maji ambayo si salama kwa afya. Benki ya Dunia imesema imekubali kuipatia Pakistan mkopo wa dola milioni 900 huku ikitahadharisha kuwa athari ya janga la mafuriko kwa uchumi wa nchi hiyo itakuwa kubwa mno. Watu wasiopungua 1,600 wamefariki dunia kutokana na mafuriko yaliyoikumba Pakistan na kusababisha wengine wapatao milioni 20 kubaki bila ya makazi

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!