Searching...
Friday, August 20, 2010

Pakistan yakubali msaada kutoka India

Waathirika wa mafuriko huko Pakistan wakipokea misaada.
Waathirika wa mafuriko huko Pakistan wakipokea misaada.
Pakistan imesema itakubali kupokea dolla milioni 5 za misaada ya mafuriko kutoka India ambayo Waziri Mkuu wa Pakistan  Shah Mehmood Qureshi ameita ni hatua inayopekelewa vizuri wakati nchi hizo mbili zikifanya juhudi ya kuboresha uhusiano wao.
Marekani ilihimiza Pakistan kukubali msaada huo wa India na kutokukubali uadui uingie kati kati ili kusaidia raia wa Pakistan million 20 walioathiriwa na mafuriko mabaya kuliko yote katika historia ya nchi hiyo.
Gazeti la Uingereza la Financial Times liliripoti Ijumaa kuwa Pakistan itaomba shirika la fedha duniani IMF kupunguza masharti ya mkopo wa dola bilioni 10.
Makala  hiyo inasema waziri wa fedha wa Pakistan Abdul Hafeez  Shaikh atasafiri kwenda Washington wiki ijayo ili kuiomba IMF kuandika upya masharti ya mkopo huo au kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo mpya.
Alhamisi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao maalum juu ya mafuriko, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kwa ukarimu raia wa Pakistan walioathiriwa na janga hilo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!