Searching...
Monday, July 19, 2010

Wataalamu watoa wito wa kutengenezwa kinga ya maradhi ya ukimwi

Sample ImageWasomi na wataalamu wa maradhi ya ukimwi wametoa wito wa kufanyika juhudi kubwa zaidi za kutumia vyema rasilimali chache zilizopo kwa ajili ya kupambana na maradhi hayo kote duniani. Wito huo umetolewa muda mfupi kabla ya kuzinduliwa mkutano wa 18 wa kimataifa wa Ukimwi ulioanza jana katika mji mkuu wa Austria Vienna. Wasomi hao wanaofanya juhudi za kutengeneza kinga ya virusi vya ukimwi wamesema kuwa hatua za kuridhisha zilizopigwa katika miaka ya hivi karibuni katika uwanja huo zinatia matumaini.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umetangaza mbinu mpya ya kutibu ukimwi ambayo huenda ikazuia vifo vya watu milioni 10 kufikia mwaka 2025. Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi unatarajia kwamba gharama za kutibu ukimwi zitapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na dawa mpya ya maradhi hayo iliyopewa jina la 2/0.
Zaidi ya watu elfu 20 wakiwemo wasomi na wataalamu wa masuala ya ukimwi wanashiriki katika mkutano huo unaojadili matumaini ya kupatikana kinga ya ugonjwa huo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!