Katika taarifa, Ban amewahakikishia Wasomali kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia ili waweze kufikia ndoto yao ya kuishi kwa amani, uthabiti na ustawi. Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmad naye ameadhimisha mwaka wa 50 wa uhuru akiwa katika mstari wa mbele vitani katika mji mkuu Mogadishu. Rais Sheikh Sharif ameonekana akiwa na magwanda ya kijeshi juu ya kifaru cha vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika. Wanajeshi wa serikali wanashirikiana na vikosi hivyo vya Umoja wa Afrika kupambana na waasi mjini Mogadishu.
Somalia ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya utawala wa rais Siad Barre Kuangishwa mwaka 1991. Somalia iliasisiwa Julai Mosi mwaka 1960 wakati eneo la kusini lililokuwa chini ya utawala wa Italia lilipojiunga na eneo la kaskazini lililokuwa likitawaliwa na Uingereza.


0 comments:
Post a Comment