Searching...
Friday, July 2, 2010

Mashirika ya Kenya yakasirishwa na wabunge kujiongezea mishahara

Sample ImageMashirika kadhaa ya kijamii yametoa taarifa ya kulaani hatua ya wabunge wa Kenya ya kujiongezea mishahara huku nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiendelea kuzongwa na umasikini. Mkurugenzi wa shirika la Kenya Moja Bw. Mathew Makori amesema kuwa kwa sasa Kenya inakabiliwa na wakati mgumu kiuchumi na kwamba hatua hiyo ya wabunge imeonyesha ubinafsi wa viongozi hao.
Wabunge wa Kenya walipitisha kwa kauli moja muswada wa kuwaongeza mishahara siku ya Jumatano ambapo sasa mshahara wa mbunge utafikia shilingi milioni 1.2 kutoka shilingi laki nane unusu. Wananchi kwa upande wao wametishia kutoshiriki kwenye kura ya maoni ya Agosti 4 kuhusu katiba mpya iwapo rais Kibaki ataidhinisha sheria hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!