
Tarehe 3 ni siku ya heshima ya Umoja wa Afrika, na shughuli za kuadhimisha siku hiyo zimefanyika katika Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai.
Naibu mkurugenzi wa kamati ya utendaji ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai Bw. Zhou Hanmin amesema, kamati ya Umoja wa Afrika ilichagua "athari kubwa ya nishati safi kwa uendeshaji wa miji ya Afrika" kuwa ni kauli mbiu ya kushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa, hali hii inaonesha ufuatiliaji wa Afrika kwa mazingira ya kuishi binadamu na mawazo ya bara hilo ya kuendeleza miji.
Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya biashara na viwanda Bi Elisabeth Tankeu ameeleza matumaini yake kuwa, kwa kupitia Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai, Afrika itapata njia mpya ya kutimiza amani na usalama mijini kwa kupitia maisha bora ya wakazi.


0 comments:
Post a Comment