Searching...
Friday, June 4, 2010

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia atangaza kung'atuka

Sample ImageAhmad Oulad Abdullah Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametangaza kuwa, atajiuzulu wadhifa huo ifikapo mwezi ujao wa Julai. Oulad Abdullah amesema kuwa, uamuzi huo haufungamani hata kidogo na matamshi ya utata aliyoyatoa hivi karibuni kuhusiana na mgogoro wa serikali ya mpito ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmad. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia aliunga mkono uamuzi wa Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmad wa kumuondoa madarakani Omar Waziri Mkuu AbdulRashid Sharmarke. Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, kuna uwezekano mkubwa kwa Ban Ki- Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumteua mwanadiplomasia kutoka Tanzania kuchukua nafasi ya Ahmad Oulad Abdullah. Taarifa zinasema kuwa, Dakta Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU huenda ndiye mtu atakayechukua nafasi hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!