
Kwenye taarifa hiyo Bw. Ban Ki-Moon alisema, Bw. Floribert Chebeya akiwa kiongozi wa harakati za kutetea haki za binadamu wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo anaheshimiwa na jumuiya ya kimataifa na ndugu zake, na kazi alizozifanya zikiwa ni alama ya moyo thabiti wa watu wa nchi hiyo zitakumbukwa na watu.
Bw. Ban Ki-Moon pia alisema, Umoja wa Mataifa unajiandaa kutoa msaada kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo kupitia Tume maalumu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

0 comments:
Post a Comment