Searching...
Saturday, June 26, 2010

Maelfu ya Waingereza hufariki dunia kwa vyakula visivyo na kiwango bora

Sample ImageKwa akali Waingereza elfu arobaini hupoteza maisha yao kila mwaka kutokana na kupatwa na maradhi ya mshituko wa moyo ambao husababishwa na utumiaji wa vyakula visivyokuwa na kiwango bora. Taasisi ya Afya ya Umma nchini Uingereza imetangaza habari hizo na kutaka kupigwa marufuku utumiaji wa mafuta ya kula ya viwandani na kusisitiza kuwa utumiaji wa mafuta hayo huleta madhara makubwa kwa afya za watumiaji wa mafuta hayo. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, utumiaji wa mafuta hayo husababisha vifo vinavyotokana na maradhi ya moyo. Taasisi ya Afya ya Umma nchini Uingereza imetahadharisha kuwa kila mwaka watu wasiopungua elfu arobaini hupoteza maisha yao nchini humo kutokana na maradhi mbalimbali ikiwemo mshtuko wa moyo, maradhi ambayo husababishwa na utumiaji wa mafuta hayo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!