Searching...
Friday, June 25, 2010

LORI LAPARAMIA GESTI, WATEJA WACHANGANYIKIWA

Lori lilivyovamia nyumba hiyo
LORI la mchanga aina ya Nissan Diesel lenye namba za usajili T 614 ASZ, leo alfajiri liliparamia nyumba ya wageni iitwayo Palm Tree, iliyopo kando ya barabara ya Kawawa eneo la Kigogo Mbuyuni, jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, baadhi wateja waliokuwa wamelala kwenye nyumba hiyo walitoka nje wakiwa wamechanganyikiwa, wengine wakiwa na vinguo vya ndani.


Mmoja wa mashuhuda akiangalia tukio hilo.


Sehemu inayoonesha jina la nyumba hiyo.


Ubao ukionyesha vyumba vipo katika nyumba hiyo.



Watu waliofika katika tukio hilo.


Katika hali iliyoonyesha watu wengine kutokuwa na shughuli ya kufanya, baadhi ya mashuhuda waliamua kukaa chini wakati wakishudia tukio hilo.
Habari na Globapublisher

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!