Searching...
Tuesday, June 1, 2010

Afrika yataka kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa


Viongozi wa nchi 38 za Afrika wamesisitiza kuwa, inabidi Umoja wa Mataifa ufanyiwe mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi muhimu zaidi nchi za Afrika.
Hayo yamekuja huku viongozi wa nchi 38 za Afrika wakitarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa 25 wa Afrika na Ufaransa huko Riviera, Nice, nchini Ufaransa.
Weledi wa mambo wanasema kwamba mkutano huo umeitishwa ili kustawisha uhusiano wa mkoloni mkongwe Ufaransa na nchi za Afrika hususan kati ya mkoloni huyo wa Ulaya na makoloni yake ya zamani ya magharibi mwa Afrika.
Mwaka 2005, nchi za Afrika zilitoa kauli ya pamoja zikitaka nchi mbili kubwa za Afrika zipewe haki ya kura ya veto katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!