
Akizungumza nchini Sweden katika kongamano la kupambana na dawa za kulevya, Bi Jenniger Kimani Mwenyekiti wa Kampenzi Dhidi ya Dawa za Kulevya Kenya amesema asilimia 68 hadi 88 ya wanaojidunga dawa za kulevya wanaugua Ukimwi. Amesema kuongezeka uraibu wa dawa za kulevya kumedidimiza mafanikio yaliyokuwa yamepatikana katika kudhibiti ugonjwa huo hatari wa Ukimwi. Wakati huo huo wanaougua Ukimwi barani Afrika wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha baada ya nchi wafadhili kupunguza misaada ya kimatibabu. Jumuiya ya Madaktari Wasiokua na Mipaka imetoa wito kwa nchi tajiri duniani kutekeleza ahadi za kuzisaidia nchi za Kiafrika kupambana na Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment