Searching...
Monday, May 31, 2010

Ki-Moon: Watu milioni moja na nusu hufariki kila mwaka kwa uvutaji sigara

Sample ImageKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema ongezeko la utumiaji wa sigara ulimwenguni linatia wasiwasi. Ban Mi-Moon amesema katika ujumbe wake kwa mnasaba wa siku ya kimataifa isiyo na uvutaji sigara inayoadhimishwa hapo kesho, kuwa kila mwaka zaidi ya watu milioni moja na laki tano hufariki dunia kutokana na uvutaji sigara. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema vingi kati ya vifo hivyo hutokea katika nchi za watu wenye pato dogo na la wastani. Ameongeza kuwa endapo hazitochukuliwa hatua za kukabiliana na uvutaji sigara, hadi mwaka 2030 kiwango hicho cha vifo kitafikia watu milioni mbili na laki tano. Aidha ujumbe huo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa umebainisha kuwa kila mwaka watu laki sita hufariki dunia kutokana na kuathiriwa na moshi wa sigara zinazovutwa na watu wengine, ambapo thuluthi mbili kati yao ni wanawake

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!