Searching...
Monday, May 31, 2010

Ban aipongeza Malawi kwa mafanikio ya kukabiliana na umasikini na njaa

Malawi lazima ijulikane duniani kote kwa mafanikio yake ya kupambana na umasikini na njaa na kuongoza katika kampeni ya malengo ya milenia.

Ban Ki-moon katika bunge la Malawi

Ban Ki-moon katika bunge la Malawi

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozungumza na waandishi wa habari mjini Lilongwe Malawi baada ya kuhutubia bunge la nchi hiyo jana. Ban amesema tunaweza na tutafikia malengo ya milenia akielezea hamasa ya kufanya hivyo ameipata Malawi. Ameongeza kuwa huo ndio ujumbe atakaoubeba kwenye mkutano wa mataifa manane tajiri duniani G-8 watakaohudhuria mkutano wa malengo ya maendeleo ya milenia mwezi wa septemba.

Malengo ya milenia yanatoa wito wa kufikia kuwa na elimu ya msingi kwa kila mtoto duniani, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake, kupunguza vifo vya watoto na kina mama wajawazito, kudhibiti ukimwi, malaria na magonjwa mengin
Idhaa ya kiswahili redio UM.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!