Takataka za sumu za Scotland zatupwa katika nchi masikini duniani
Scotland kila mwaka hutupa maelfu ya tani za takataka za sumu zilizozalishwa katika viwanda na vituo vya kibiashara katika nchi masikini duniani. Kanali ya Televisheni ya Press TV imetangaza kuwa, takataka hizo za sumu zinajumuisha pia magurudumu yaliyoraruka na makaratasi, ambazo kila mwaka hutupwa katika nchi za Nigeria, Ghana, Indonesia, Pakistan na Zanzibar. Taarifa hiyo imeeleza kuwa takataka hizo hutishia mazingira na afya za wananchi wa nchi hizo. Taasisi ya Hifadhi ya Mazingira ya Scotland imeeleza kuwa, baadhi ya wafanya magendo huzihamishia takataka hizo za sumu kwenye nchi hizo. Taasisi hiyo imeeleza kuwa hadi sasa nchi za Scotland, Uingereza na Uholanzi zimefanikiwa kuzuia shehena nane za takataka za sumu tokea ulipoanza mwaka huu na hali kadhalika ziliwahi kuzuia upelekwaji wa shehena nne za sumu mwaka 2008.
0 comments:
Post a Comment