Utumiaji mbaya wa watoto unazidi kuongezeka nchini Marekani
Watetezi wa haki za watoto wamesema maafisa wa vyombo vya sheria nchini Marekani hawachukui hatua za maana kuzuia na kupambana na utumiaji mbaya wa watoto nchini humo. Ernie Allen, Mkuu wa kituo cha taifa kinachoshughulikia watoto ambao hawajulikani waliko na wale waliotumiwa vibaya NCMEC amezikosoa taasisi na vyombo vya sheria vinavyohusika na masuala hayo akisema kuwa vyombo hivyo havichukui hatua za haraka zinapotolewa ripoti za kutoweka na kupotea kwa watoto. NCMEC inashughulikia na kuwatafuta watoto waliotoweka pamoja na kuelimisha jamii juu ya namna ya kukabiliana na utekaji nyara na utumiaji mbaya wa kijinsia wa watoto hao. Kwa mujibu wa kituo hicho, kila mwaka kati ya watoto 100,000 hadi 300,000 hufanyishwa vitendo vya ukahaba kwa nguvu nchini Marekani ambapo baadhi ya watoto hao wana umri wa miaka 12 tu
0 comments:
Post a Comment