Pakistan imesema itakubali kupokea dolla milioni 5 za misaada ya mafuriko kutoka India ambayo Waziri Mkuu wa Pakistan Shah Mehmood Qureshi ameita ni hatua inayopekelewa vizuri wakati nchi hizo mbili zikifanya juhudi ya kuboresha uhusiano wao.
Marekani ilihimiza Pakistan kukubali msaada huo wa India na kutokukubali uadui uingie kati kati ili kusaidia raia wa Pakistan million 20 walioathiriwa na mafuriko mabaya kuliko yote katika historia ya nchi hiyo.
Gazeti la Uingereza la Financial Times liliripoti Ijumaa kuwa Pakistan itaomba shirika la fedha duniani IMF kupunguza masharti ya mkopo wa dola bilioni 10.
Makala hiyo inasema waziri wa fedha wa Pakistan Abdul Hafeez Shaikh atasafiri kwenda Washington wiki ijayo ili kuiomba IMF kuandika upya masharti ya mkopo huo au kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo mpya.
Alhamisi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao maalum juu ya mafuriko, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia kwa ukarimu raia wa Pakistan walioathiriwa na janga hilo.
0 comments:
Post a Comment