Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Nigeria, Ibrahim Babangida, ametangaza kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Amesema kutokana na uzoefu wake ana uwezo wa kukabiliana na matatizo ambayo yanaikumba nchi hiyo. Babangida aliitawala nchi hiyo kati ya mwaka 1985 hadi 1993 baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi.
Baada ya kustaafu alikabidhi uongozi kwa serikali ya muda.
Pamoja na Babangida kiongozi mwingine muislamu kutoka kaskazini mwa nchi hiyo anayepania kuchaguliwa na chama tawala cha People's Democratic Party kwa teketi hii ya urais ni aliyekuwa makamu wa rais, Atiku Abubakar.
Rais wa hivi sasa, Goodluck Jonathan -- aliyechukua hatamu za uongozi baada ya kifo cha rais Umaru Yar'Adua mwezi Mei mwaka huu hajatangaza kuwania kiti hicho hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment