Searching...
Monday, July 19, 2010

Watu wasiopungua 48 wafariki dunia katika ajali ya treni India

Sample ImageWatu wasiopungua 48 wamefariki dunia katika ajali ya treni mbili zilizogongana huko mashariki mwa India mapema leo Jumatatu. Afisa mmoja wa serikali ya India amesema ajali hiyo ilitokea baada ya treni ya abiria kugonga treni nyingine iliyokuwa imesimama katika mji wa Sainthia kwenye jimbo la Bengal Magharibi.
Watu wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa katika ajali hiyo.
Sababu ya ajali hiyo bado haijajulikana na kuna uwezekano idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeruhi.
Baadhi ya vituo vya televisheni vya India vimetangaza kwamba idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni kati ya 70 hadi 100.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!