Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesisitiza kuwa katiba mpya ya nchi hiyo hataikuwa na kipengee chochote kinachodhamini haki ya kuruhusu ndoa za watu wa jinsia moja. Mugabe amenukuliwa na vyombo vya habari vya Zimbabwe akisema Wazimbabwe hawatasikiliza maneno ya watu wanaotoa wito wa kuruhusiwa ndoa kati ya watu wa jinsia moja. Kiongozi huyo mkongwe wa Zimbabwe, kama walivyo viongozi wengi wa Afrika, anapinga vikali mahusiano yoyote ya kujamiiana kati ya watu wa jinsia moja na amekuwa akiwataja watu wa aina hiyo kuwa ni sawa na mbwa na maguruwe.
Serikali ya Zimbabwe inayatarisha rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura ya maoni mwaka ujao.
Nchi za Magharibi zinaishikiza Zimbabwe kudhamini haki ya kuruhusu ndoa kati ya watu wa jinsia moja katika katiba mpya ya nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment