Ofisa mwandamizi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres ambaye yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo tarehe 21 Julai aliitaka jumuiya ya kimataifa ifuatilie wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, na kutoa msaada kwao.
Alisema wakimbizi hao wanakabiliwa na tatizo la ajira, elimu na matibabu. Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufuatilia zaidi sehemu hiyo, na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pia inapaswa kuchukua hatua zenye ufanisi zaidi kutatua masuala hayo.
Aliongeza kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kulinda hali ya usalama ya huko, na kuwawezesha wakimbizi waliokimbilia katika nchi nyingine kurudi nchini kwao.
0 comments:
Post a Comment