Bodi ya wakurugenzi ya shirika la fedha duniani IMF imeidhinisha kuifutia Haiti deni lote la dola milioni 268 inalodaiwa na shirika hilo.
Bodi hiyo pia imeidhinisha mipango ya miaka mitatu ya kuiongezea mkopo nchi hiyo kutokana na ombi maalumu la serikali.
Fedha za deni lililofutwa na mkopo itakaoongezewa zote zitatumika katika ujenzi mpya wa nchi hiyo ambayo ilisambaratishwa vibaya na tetemeko la ardhi mapema mwaka huu.
IMF inasema uamuzi huo umefuatia tathimini ya kina kuhusu hali halisi inayoikabili Haiti ambapo mamilioni ya watu bado wanaishi kwa kutegemea msaada, mfumo wa serikali haujitoshelezi na miundombinu na uchumu vyote vinatakiwa kufufuliwa upya.
0 comments:
Post a Comment